Jumatano, 7 Aprili 2021

flavianamatata Verified Mama yetu, Mhe. @samia_suluhu_hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Top Talent

Mama yetu, Mhe. @samia_suluhu_hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wewe ni kioo kwa watoto wote wa kike hapa nchini na Afrika nzima. Wewe ni taswira halisi ya yale yote ambayo sisi Wanawake tunaweza kufanya tukiaminiwa, tukijiamini na kupata nafasi.

Wewe ni alama ya ushindi. Najivunia kusema wewe ni Rais wetu na ndio maana niliomba na kusisitiza kwamba mimi mwenyewe ndiyo nitundike picha yako hapa ofisini kwetu.

Kama wewe ulivyopanda kuanzia chini ukaweka historia kwa kuwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke (Tanzania) na sasa Rais wa Kwanza Mwanamke hapa Tanzania, ndivyo mimi nilivyopanda ngazi hii kuiweka picha yako. Wewe ni alama ya ukuaji kuanzia chini hadi juu.

WE ARE SO PROUD OF YOU NA TUNAKUOMBEA SANA MWENYEZI MUNGU AKULINDE. #WomenInPower #WomenInPolitics


Hakuna maoni:

Layout

Mtua Studio- Photo Shoot

Top Talent