Msanii Steve Nyerere amefunguka baada ya kuandamwa sana katika mitandao ya kijamii kuhusu kauli yake ya kuwa Ommy dimpoz hawezi kuimba tena kwa sababu ya upasuaji aliofanya nchi Afrika ya Kusini.
Msanii huyo ambae aliwahi kuojiwa akiwa kama moja ya watu wanaoshughulikia sana matatizo ya wasanii alisikika akisema kuwa Ommy hawezi tena kuimba kwa sababu koo lake halina tena uwezo huo kutokana na malazi yanayomsumbua.

Hata hivyo msanii huyo amerudi kutoka katika matibabu hivi karibuni na kusema kuwa maneno hayo aliyasikia lakini anaamini kuwa hiyo ni moja ya changamoto anazop[itia kikubwa anamshukuru mungu kwa kuwa amefanya arudi tena katika kazi yake.






