BENDI ya African Stars “Wana Twanga Pepeta” imezindua albamu yake 10 ijulikanyo kwa jina la Nyumbani Ni Nyumbani kwenye viwanja vya Leaders Club huku ikisherehekea miaka 15 tokea kuanzishwa kwake.
Uzinduzi huo uliambatana na michezo mbali mbali kuanzia saa 3.00 asubuhi ambapo timu nane za mpira wa miguu zitawania zawadi mbali mbali katikamichuano ijulikanalo kwa jina la ASET Bonanza. Timu hizo ziliongozwa na ile ya waandishi wa habari za michezo, Taswa FC na nyingine kama Brake Point, Mango, Namanga, Kivukoni, Camp Combine, Wagadau na Kunduchi.
Mbali a burudani kutoka kwa Twanga Pepeta, siku hiyo pia ilikuwa na burudani kutoka kwa wanamuziki wa kizazi kipya, Linex, Barnaba, bila kusahau, wakongwe wa muziki wa dansi nchini, bendi ya Mlimani Park maarufu kwa mtindo wa Sikinde Ngoma ya Ukae.
Albamu nyingine za bendi hiyo ni Kisa Cha Mpemba iliyozinduliwa mwaka 1999, Jirani (2000), Fainali Uzeeni (2001), Chuki Binafsi (2002), Ukubwa Jiwe (2003), Mtu Pesa (2004), Safari (2005),Password (2006), Mtaa wa Kwanza (2007), Mwana Dar es Salaam (2009) na Dunia Daraja iliyozinduliwa mwaka 2011.
Asha alisema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuwakumbusha mashabiki wao wapi walipoanzia (tokea) na wapi wanapokwenda katika muziki wa dansi. Alisema kuwa kimuziki wamepata mafanikio makubwa sana kutokana na kupata mialiko ya kimataifa kama nchi za Ulaya mama Uingereza, Ujerumani, Uholanzi, Finland, Norway na nyingine nyingi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni