Jumatano, 10 Julai 2013

TOA SUPPORT KWA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU VETERAN TEMEKE!

Top Talent
Katika ule mradi niliouelezea wa Dada Dina Cares nilipata nafasi ya kwenda temeke vetenary na kukutana na mwanamke huyu pichani.Mwanamke huyu ni mwalimu wa chekechea mlezi wa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi.Kihistoria ni mzaliwa wa mkoa wa Morogoro ambae alipata ulemavu akiwa mdogo baada ya kuugua ugonjwa wa polio anaitwa Honoratha Soud.Akiwa mdogo aliugua polio iliyopelekea kupata ulemavu mpaka leo.Hajaolewa na wala hana mtoto ila analea wadogo zake wawili na bibi yake baada ya wazazi wote kufariki.

Nilivyofika tu nikapata rafiki anaitwa Ad ni mcheshi kiutoto utoto tunasema mtundu nae analelewa na Honoratha.Honoratha alisukumwa kulea watoto kulingana na mazingira aliyokulia.Kuwa mlemavu katika familia maskini tena kijijini alikijuta akitengwa sana mpaka walipotokea wazungu wakamchukua kutoka kwa wazazi wake na kumuweka katika vituo kumlea na kumsomesha.Alinitajia kituo hicho nimekisahau ambacho wazungu hao walishaondoka ila walimuacha akiwa na elimu na uwezo wa kujisimamia.Elimu inayomsaidia mpaka leo kwani ni mwalimu wa chekechea na anashule yake mwenyewe.

                                           Nilikuta watoto wanakula chakula cha mchana
 Honoratha anaweza kuendesha maisha ya watoto kwa ada anayopata pia kilimo.Anasema zamani alinunua shamba mkoani mbeya anakojishughulisha na kilimo cha mpunga na maharage.Akivuna anauza pia kupata chakula cha wanawe.

Shule hiyo ndio anafundisha watoto wake yatima na wamazingira magumu na wale wenye wazazi.Wenye wazazi ndio wanalipa ada Tsh 10,000 kwa mwezi.Madarasa hayo usiku ndio wanatandika magodoro wanalala asubuhi wanakunja na kuwa shule.Aliweza kununua kiwanja na akajenga kwa msaada wa mdogo wake ambae ni fundi ujenzi.

Wadada wanaowasimamia watoto kwa kuwapikia,kuwaogesha,kuwalisha n.k
                     Wadada wanaowasimamia watoto kwa kuwapikia,kuwaogesha,kuwalisha n.k
                                           Kwa nyuma huko ndio stoo na wanakoweka magodoro
Bado sijatoa utaratibu wa wadau wangu wa blog mtachangia nini,kwa sababu nafikiria kiwe kitu kimoja au viwili vya msingi.
Nakaribisha maoni pia kwa dina_marios@yahoo.com
 Nilimkuta mdogo wa Honoratha akifanya ujenzi wa chumba ambacho wanatarajia ndio kiwe cha watoto kulala moja kwa moja.Sio kulala usiku asubuhi darasa.Challenge ndio vitanda,magodoro,mashuka,na vyandarua na madirisha kuyaweka nyavu ili watoto wasing'atwe na mbu.Amejitahidi mwenyewe kajenga vizuri kweli na mimi nikamuahidi tutamtimizia hayo.Mdogo wake huyu anamsaidia sana linapokuja swala la kujenga na ufundi wa vitu mbalimbali.
 Bado sijatoa utaratibu wa wadau wangu wa blog mtachangia nini,kwa sababu nafikiria kiwe kitu kimoja au viwili vya msingi.
Nakaribisha maoni pia kwa dina_marios@yahoo.com

 Hapo ana watoto ambao wanalelewa na bibi baada ya wazazi kufa na bibi hajiwezi kwa lolote.Analea watoto ambao wazazi wapo lakini hawana uwezo wa kufanya chochote kwa watoto wao hivyo kuishi katika mazingira magumu na hatarishi pamoja na wale yatima.
Nilichomuahidi ni vitanda,mashuka,magodoro,vyandarua,nyavu kwenye madirisha,sabuni za kufua na kuoga,dawa za meno,mafuta ya kujipaka,nguo na chakula.

Bado sijatoa utaratibu wa wadau wangu wa blog mtachangia nini,kwa sababu nafikiria kiwe kitu kimoja au viwili vya msingi.
Nakaribisha maoni pia kwa dina_marios@yahoo.com

Baada ya maongezi nikaondoka na mama akanisindikiza.Nashukuru baada ya kuongelea Dada Dina Cares respond imekuwa kubwa namshukuru Mungu kwa hilo naamini tutafanikisha.
Kila mmoja moyo wake unasukumwa kushiriki kujitolea kwa hali na mali.Pia nashukuru wale mlioniandikia kwa kunipa mawazo/ideas mbalimbali.

Hakuna maoni:

Layout

Mtua Studio- Photo Shoot

Top Talent