Alhamisi, 28 Machi 2013

MATAMASHA YA AIRTEL YATOSHA KUFANYIKA NCHI NZIMA

Top Talent

KAMPUNI ya simu ya Airtel imezindua matamasha maalumu yenye lengo la kutoa burudani na kuielimisha jamii na wateja wake juu ya huduma zake mbalimbali ikiwemo huduma mpya ya Airtel Yatosha inayomwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa gharama nafuu zaidi.

Akizungumza wakati wa kutambulisha matamasha hayo jijini Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema wameamua kutoa burudani wakati wa msimu huu wa sikukuu, ikiwa ni pamoja na kuitambulisha huduma ya Airtel Yatosha.

“Safari yetu ya burudani za Airtel Yatosha itaanza katika Mkoa wa Morogoro Jumapili na Jumatatu, kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni pale katika viwanja vya Sabasaba,” alisema.

Mmbando aliwataja wasanii watakaotumbuiza kuwa ni Farid Kubanda ‘Fid Q’, Juma Kassim ‘Sir Juma Nature’, Ney wa Mitego na Tip Top Connection ambako kiingilio kitakuwa ni bure.

“Tunapenda kukualika wewe na washikaji zako wote kuhudhuria katika tamasha hili la kwanza kabisa pale Morogoro na utapata burudani kabambe. Njoo na kitambulisho chako ili uunganishwe na ufurahie ofa nyingi toka Airtel,” aliongeza Mmbando.

Kiongozi wa Tip Top Connection, Hamad Ally ‘Madee’ alisema kama kawaida wamejipanga kuwapa wateja wa Airtel na Watanzania burudani ya ukweli katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, hivyo wanawaomba wajitokeze kwa wingi katika matamasha hayo ya Airtel Yatosha.

“Mbali na sisi kutoa burudani, itakuwa nafasi pia kwetu kuona vipaji mbalimbali vya mashabiki wetu ambao ndio wasanii nyota wa kesho, hivyo tunawapa hamasa ya kujitokeza kwa wingi ili tuweze kuburudika pamoja,” alisema Madee.

Wasanii watakaoshiriki matamasha maalumu ya Airtel Yatosha wanatamba na vibao mbalimbali kama ‘Sihitaji Marafiki’ cha Fid Q, ‘Nasema Nao’ wa Ney wa Mitego huku Tip Top Connection wakitesa na ‘Nani kamwaga pombe yangu’.

Hakuna maoni:

Layout

Mtua Studio- Photo Shoot

Top Talent