Jumatano, 22 Aprili 2020

Maneno ya k2ga kwa Mashabiki zake....! @officialalikiba ni Mikono salama sana kwa maisha na muziki wangu,

Top Talent

Ndugu Mashabiki zangu wapenzi nimepata meseji nyingi na simu nyingi pamoja na comment zakutosha sana kutoka kwenu wote mkiulizia juu ya hatima yangu!
NI HIVI
Naamini sana katika ndoto vile vile naamini sana katika Alikiba !
Mashabiki msinitilie shaka hata chembe @officialalikiba ni Mikono salama sana kwa maisha na muziki wangu, nanyi mashabiki zangu mzidi kuniombea niweze shinda vita hii,
Najua mmehuzunika hata mimi pia nimehuzunika, nimepata wakati mgumu mno kwa muda wa wiki moja sasa,
Kila nikitaka kuandika nafuta, niliandika nikafuta zaidi ya mara kumi!

Hatimae Kwa Utashi wangu nilopewa na Muumba na kwa unyenyekevu mbele yenu mashabiki nimeamua kubaki @kingsmusicrecords (Kama Location inavyosoma hapo juu)

Kusema ukweli nampenda Mno Alikiba sana nawahusudu mashabiki zangu,
Ni YEYE alinitambulisha kwenu akanifungulia Dunia na kwa moyo wake wa upendo mmenipokea kwa mikono miwili, naomba sana ndugu zangu muendelee kubaki na mimi ,
enyi mashabiki watukufu Muombeeni @officialalikiba asinichoke aniongoze mdogo wake kwenye safari hii ngumu ambayo yeye ndio anajua njia,
Mimi bado mgeni kwahiyo kando ya MOLA nawategemea sana nyinyi pamoja na yeye nawatakia Maandalizi mema ya ramadhan na jiandaeni kupokea zawadi. Ahsanteni 

Hakuna maoni:

Layout

Mtua Studio- Photo Shoot

Top Talent