Jumatano, 22 Aprili 2020

Cheed na #Killy hawafanani bora hiyo kauli angeongea Killy,

Top Talent

Okay, sema Cheed unachoongea naamini kwa upande wako upo sahihi lakini kwa muda huu unaharibu sana, Chunga sana kauli unazotoa kwa sasa kwenye Media.

Now mnaweza kuona mnafuatwa sana na Media ni sababu hata kwao Media kwa sasa nyinyi mmekuwa ni habari, tena habari kubwa tu. Mnapoongea shit yoyote now ni faida kwa Media.

Majuzi nimemsikia Cheed anasema yeye ameanza ku husle kabla hata ya Cinderella" 😀😀😀 Kiutu uzima alikuwa anapinga kauli kwamba yeye ametokea Kings Music Label yaani tumemjua hapo, So anaonesha kwamba ameanza ku husle tangu muda.

Yuko sahihi maana ukweli anaujua mwenyewe na watu wake wa karibu, Ila kuna mambo ni kama utoto hivi 😀😀 Mfano unakutana na mtu amefulia anaanza kukwambiaaa aisee mimi zamani nilikuwa na hela sana yani 😀😀 Swali, So?? Kama ulikuwa na hela ziko wapi now?? Unataka kusema nini?? Unajifariji...Yaani.

Cheed ajifunze kitu kwa Harmonize, Najua kulikuwa na mengi chini ambayo mengine yalikuwa mabaya kwa Harmo lakini nimependa bado ana praise upande wa pili na watu wanatamani kama aanzishe nao bifu lakini kila ukimsikia Hamo yupo vyema sana kwenye kupangilia anachoongea, instead anapiga madongo kibiashara kama ngoma ile Hainistui....Kama ningekuwa mimi mshauri wa Killy Na @officialcheed kwa sasa ningekataa wafanye Interviews.

Ningewaambia wakae kimya kwa muda kama wa miezi miwili mpaka mitatu then waje na ngoma back to back kama 03 hivi hapo ndio ruksa sasa kuanza interviews..Katika hizo interviews zingetazamwa zaidi maana watu wangekuwa wanataka kujua wanasema nini kuhusu AliKiba...Hiyo kutaka kujua wanasema nini automatic inge boost nyimbo zao.

@officialkilly_tz nimependa sijaona akiongea maneno controversial' ila Cheed alafu Cheed na #Killy hawafanani bora hiyo kauli angeongea Killy, Cheed mzee Baba bado una safari ndefu sana aisee binafsi I (We) don't give a F* hata kama ulianza ku husle kabla ya Cinderella, Hiyo ni non of our business sisi tunataka utuoneshe kile Boss wenu alichofeli kuhusu wewe wakati ukiwa Kings.

Honest Nitaendelea kuwapa support 100% but kazi zioenekane
.
.
.
.
.
#kingkiba #youngking #kingsmusic4life

Hakuna maoni:

Layout

Mtua Studio- Photo Shoot

Top Talent