KAMATI YA WAZIRI NAPE YAKABIDHI RIPOTI MAKONDA KUVAMIA CLOUDS..KAMATI IMEBAINI MAMBO HAYA...YAPO MAPENDEKEZO
Tulifanya mahojiano na wafanyakazi 14 wa kituo cha Clouds-Balile
Tulifanya jitihada za kumtafuta Mkuu wa Mkoa, tulimpigia simu lakini hakupokea.- Balile
"Hata tulipofika katika ofisi yake, aliondoka kupitia mlango wa nyuma". -Balile
"Baada ya kushindwa kuonana naye, tukajiridhisha kuwa amechagua mwenyewe kutotumia fursa ya kuhojiwa". -Balile
"Katika uchunguzi wetu, tumejiridhisha kuwa Mkuu wa Mkoa alivamia kituo cha Clouds akiwa anaendesha gari mwenyewe". -Balile
"Kamati imejiridhisha kuwa RC na askari wenye silaha waliingia hadi ndani ya studio iliyokuwa ikirusha matangazo". -Balile
'Imebainika ni kweli alikwenda pale Clouds na askari, waliingia kwenye vyumba ambavyo walipaswa kuingia kwa idhini maalumu'-Balile
"Kamati imejiridhisha pia kuwa palikuwa na vitisho kwa walinzi na wafanyakazi kwa kutumia askari wenye silaha". -Balile
"Miongoni mwa vitisho ni kuwalazimisha kurusha kipindi vinginevyo angewaingiza kwenye tuhuma za dawa za kulevya". Balile
“Makonda aliwatishia wafanyakazi Clouds kuwa angewafunga miezi 6 pia angewaingiza kwenye orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya”-Balile
"Baada ya hapo aliwatisha kuwa yote yaliyotokea usiku ule, yabaki pale pale ndani" - Balile
"Tumejiridhisha kuwa RC Mkuu wa Mkoa aliingilia taratibu za uhariri kwa kulazimisha habari anayoitaka iruke" - Balile
"Kamati haikuona uthibitisho wowote kuwa kuna wafanyakazi waliopigwa na vitako vya bunduki au kupigwa mitama lakini walilia kwa vitisho vya kufungwa jela miezi sita bila kupitia mahakamani" - Balile
Tume Imebaini nini?,Mapendekezo Je??
ENDELEA KUSOMA HAPA>>>> https://goo.gl/h1rgd3
Habari wakuu,
Ile kamati iliyoundwa na Nape Nnauye ya masaa 24 inawasilishwa leo, baada ya kuzungumza historia ya tatizo, msemaji anasema wamejaribu juhudi zote za kumpata mkuu wa mkoa wa Dar ikiwemo kumpigia simu na kumpelekea taarifa ofisi.
Kamati imesema waliitwa ofisi ya mkuu wa mkoa na kuelekezwa ngazi za kutumia, lakini mkuu wa mkoa alitumia ngazi nyingine kutoka ofisini kwake na kuwatoroka.
Amesema Makonda aliingia kwenye studio ambazo hakutakiwa kuingia, kamati imethibitisha kulikuwa na vitisho ikiwemo kushika silaha za moto na kuwatishia kuwafunga jela miezi sita.
Pia alitoa vitisho kuwa angewakagua kama wanahusika na dawa za kulevya au wadhamini. Alitoa vitisho kwa wafanyakazi waliokuwa zamu na kusisitiza iwapo wangesema kilichotokea, wangejua yeye ni nani.
Ni kweli kwamba Makonda ana kawaida ya kwenda Clouds, mgeni mwenyeji. Ameshawahi kukaa wakati wa kuandaa kipindi chake cha mwaka mmoja mpaka saa 10 alfajiri.
Kamati haikuona uthibitisho wa wafanyakazi kupigwa au kukatwa mitama isipokuwa waliolia walitishiwa kwenda jela miezi sita bila kupitia mahakama.
Paul Makonda anatakiwa kuomba radhi, Waziri Nape Nnauye awasilishe malalamiko kwa mamlaka yake ya uteuzi
Vyombo vya dola vichunguze askari wake kuingia studio na kuepusha tukio hilo kujirudia siku za usoni.
Clouds ipitie upya miongozo yake na kuzuia watu wanaoingia mara kwa mara chumba cha habari ilhali hawana taaluma ya uhariri.
==========
NAPE: Hata mimi nilikuwa napata presha kubwa, sikujua kama lingekuwa na presha kubwa hivi. Nitoe wito watanzania wakati mwingine kuwa wavumilivu, watu walisema mambo mengi sana jana.
Nimeipokea ripoti na kazi hii ina gharama sana ikiwemo ya kusimamia haki na ukweli.
Juu yangu kuna waziri mkuu, makamu na Rais mwenyewe, nitachofanya ni kukabidhi kwao wenyewe na kama kuna chochote cha kufanya, watafanya chochote. Tunalipwa kwa pesa za walipa kodi na wavuja jasho, niwaombeni wanahabari tuendelee kuwa wavumilivu, Rais ana nia njema na tasnia ya wanahabari na sheria ya vyombo vya habari imewezekana chini ya utawala wake.
Nina imani madhaifu yakitokea kwa mtu mmoja mmoja haiwi tope kwa serikali nzima. Nyinyi ni sehemu muhimu katika kufanikisha sera, tumuunge rais mkono.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni