Jumatatu, 6 Februari 2017

Kamanda Siero kasema baada ya kumuhoji walifanya upekuzi nyumbani kwake na kukuta kuna msokoto wa bangi na kifungio. Chanzo: ITV Habari

Top Talent
Yaani mfanyabiashara wa madawa ya kulevya aliyetangazwa kwa swagger zote utadhani Pablo Escobar afu anakutwa na kamsokoto kamoja wa BANGI..??????
Afu wamejuaje ni ka kwake? 
     

Maoni ya wananchi Na maswali juu ya hili sakata la wema na dawa za kulevya'

1. Huu utani sasa. Yaani tumeaminishwa issue unga kumbe bangi.

2. Hii ndio Tanzania.

Usipokutwa na kosa polisi utatafutiwa kosa, na mara nyingi watampa mtu kesi ya kukutwa na bangi, silaha au madawa ya kulevya ili tu wasionekane wameshindwa.

3. mimi nilivyosikia ITV nilidhani nimesikia vibaya kumbe kweli

4.  hii serikali ina mambo, sasa kule kumtangaza kote kosa ni bangi?? Nakumbuka kuna mbunge wa CCM alisema bangi hialalishwe vp yule walimfanya chochote?? Mnaovuta bangi mjiandae tena mpo wengi sana

5. Police wa bongo bn

6. Juzi mara walikamata shamba zima la bangi.Sikuona mtu aliyetoa povu kama tubangi twa wema.Hii vita itawaumbua,

7. Mmmh. Mtu kaitwa siku kabla, kweli atawacha ushahidi wazi Kwake? Bongo ni shule tosha

8. sauti ya wema leo asubuhi ilisema wali sachi nyumbani kwake na hawakukuta chochote!
very interesting war ya drugs....

9. Kutoka movie ya unga hadi bange ...... 
wamefanya nimekakumbuka ka wimbo ka 20%..
....bange bange bange imesababisha nikutoroke....


10. Daaaahh tunapoelekea.... 

Mtanzania anachekelea mwenzie kufungwa bila kufuata sheria. Ila siku yakimkuta yeye au ndugu yake atakua kutafuta huruma humu 

Kumbuka walianza na Mafao yenu, wakaja kwenye haki zenu za privacy, wakaja kwa haki zenu za kisiasa na sasa wanapoelekea....

11. Hawawezi kuwa serious!
just msokoto mmoja wa bangi!
sasa yeye ni mtumiaji au muuzaji?
na hiyo ndio kusema amekutwa nao au umekutwa nyumbani kwake?
walipoenda nao kusaka nyumbani mbona hazikuja report hizo kuwa kuna chochote kimeonekana nyumbani kwao?

tunawatakia kila la heri viongozi wetu ktk kazi hii ngumu!

12.Yaani nachoka kabisa,mbona mwenyekiti wa CCM Geita alitoa ombi kwamba hili jani liharalishwe!

13. Wema smokes wee!
Aisee naacha rasmi leo, dharau staki.

14. Any way ka msokoto ka bangi tena sio kete za unga wamhekapotezea siye tunataka wauza unga ma big fish.
ningesikia kuwa wamemkuta na unga hata kete moja ngeelewa

15. Naona na humu kuna team wema wanamtetea hao balaa

16. Si tulitangaziwa ni mtuhumiwa wa kutumia sembe,kumbe sembe imegeuka kuwa weeds tena,hahahaha kama weeds basi jela itajaaa

17. Cha ajabu huu uzi binadamu tulivyo na roho za chuki tutapita kama hatuuoni. Na wakat ule uzi ya kwamba Wema ndo papa wa kuuza unga una comments zaidi ya elfu moja. Wivu tu ndo unatusumbua maskini.

18. Mthumiwa mkuu ana msokoto mmoja wa bhangi!! Amazing!

19. Bongo watu wana Roho mbaya ya kuharibiana mambo utadhani ndio wale walio msurubu Yesu ndio wametupwa hapa w

20. Haikuna kitu ni usanii na kukurupuka bila uchunguzi

21. Sizan kama mtumiaji wa madawa anaweza kukaa na msokoto mmoja tu wa bangi. Hebu kuweni na upelelezi wa maana

22. Huwajui watz kwa roho mbaya? Hapa walitamani hata angeekewa ili tu akomeshwe.

23. Only in tz

24.Mwisho wa siku haya mambo yataonekana kama mzaha...

25. ila wema katoboa siri, tulikuwa hatujui kumbe kuna baadhi ya watumiaji na wahusika hawaguswi sababu wana mahusiano au ni vimada wa muanzisha movie? Rai yetu haki itendeke kama kweli muanzisha movie ana dhamira ya kweli a deal na wote na sio kubagua otherwise afanye mambo ya msingi aachane na kukamata mateja na mapapa na wauzaji anaogopa.

26. Nchi masikini yapili kutoka chini viongozi tuliowapa thamana ya kutuongoza badala ya kutuletea maendeleo wao wapo busy kutafuta kiki kwenye mitandao kwa vitu vya hovyo kabisa mwenye mji wake anajitia muokovu kumbe mzinifu hawa watu wanajitia wachamungu na kujionyesha mbele zawatu waoniwachamungu ni wanafki sana mwl nyerere aliwai kusema kunamiko ya uwongozi sio kiongozi anafanya vitu vya hovyohovyo tu kutafuta umarufu au cheo huyo hatufai tunataka mtu mwenyeupeo wamaendeleo sasa watu wanaumbuka maana ukiwa muongo usiwe msahaulifu unapiga vita vya madawa kumbe kimada ndiye punda wa kubeba madawa sjui alisahau au vipi



27. Ukiona jeshi linatumika kisiasa ujue nchi imepoteza uwelekeo kiutawala n kiuchumi

28.Kweli Mheshimiwa Nape aliona mbali aliposema busara zitumike kwenye hili la kushughulikia wadau wa madawa ya kulevya.

29. Dah kumbe ni kosa kuwa na msokoto wa cha Ar????? Basi huku wote tutafungwa maana machalii wanapuliza mbaya
30. Mkuu bangi imewekwa kwenye kundi la madawa ya kulevya sheria iliyopitishwa 2015 hukumu yake si chini ya miaka 

31. Jela na faini ikibidi 
Kufupisha story ukikutwa na bangi na aliyebaka mnakula mvua sawa

32. Kabisa nadhani wema wamempandikizia maana watu wote walikuwa wanasubiri Kama bangi mbona wasanii wengi Sana wanavuta bangi

33. Huu ni mpango mahsusi wa kurekebisha maadili ya vijana bongo, hawa watu maarufu wana wafuasi mazombie wengi sana ambao wakiona star wao anavuta shisha au kula dawa nao wanaiga,sasa kwa kuwarudisha hawa role model kwenye mstari unaokoa wengi

34. Mkuu polisi wa bongo waje kwako wakose kitu, sahau!

35. Wametupotezea muda tu Lusaka kick
Upuuzi mtupu.






Hakuna maoni:

Layout

Mtua Studio- Photo Shoot

Top Talent