‘Sio makafiri wanaopotosha ummakuwa Nasib kumuoa Ally sio ndoa Batili’
Msanii wa muziki wa bongo flava nchini, Baghdad amesema kuwa jamii isimuelewe vibaya kutokana na kuwataja nyota wakubwa wa muziki nchini, Diamond na Ali Kiba katika ngoma yake mpya inayoitwa ‘Ninae’.
Baghdad amesema kuwa katika ngoma yake hiyo ya kimapenzi ametaja majina mawili ambayo ni Nasib na Ally lakini hakumaanisha wasanii hao wakubwa kwa kuwa nao wanatumia hayo.
Ngoma hiyo iliyotengenezwa na Isam Touches wa Kaburu Records imezungumza mambo mengi mazuri ya ndoa lakini msitari mmoja unaosema ‘Sio makafiri wanaopotosha ummakuwa Nasib kumuoa Ally sio ndoa Batili’ umemfanya mpaka aombe ushauri kwa wadau wakubwa wa muziki huo kwani ulizua kelele baina ya watu.
Baghdad ameongeza kuwa hayupo katika game kwa kuchochea bifu ndio maana kaamua kufafanua mapema kuwa hakuwalenga wasanii hao kwani hizo ni njia tu za kuapnga vina na mizani katika wimbo.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni