Jumanne, 26 Novemba 2013

Mwaka Mmoja umetimia tangu Sharo Milionea Afariki kwa ajali ya gari


Mchekeshaji na Mwanamuziki wa Bongo Fleva,Hussein Mkieti aka Sharo Milionea leo ametimiza mwaka mmoja tangu alipofariki kwa ajali ya gari iliyotokea siku kama ya leo (November 26) majira ya saa mbili usiku.

Sharo alikuwa safarini akitokea Dar es Salaam akielekea nyumbani kijiji cha Lusanga,Muheza mkoani Tanga kwaajili ya kumpelekea Mama yake mzazi fedha za matumizi.

Msanii huyo alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T478 BVR na kupata nalo ajali katika eneo la Songa-Maguzoni wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Angalia hii video hapa kutoka Millardayo.com ufahamu ajali ilipoanzia mpaka mauti yalipomkuta Sharo Milionea.

Hakuna maoni:

Layout

Mtua Studio- Photo Shoot

Top Talent